Ubalozi uliamua kuadhimisha Miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kutangaza bidhaa na vivutio vya Utalii vya Tanzania; Kukabidhi vyeti kwa Wadau mbali mbali kuonesha kutambua mchango wao katika Maendeleo ya Uchumi wa Tanzania ikiwemo Sekta ya Utalii, Uwekezaji, Sanaa, Lugha na Utamaduni . Hafla hiyo ilifanyika tarehe 26 April 2019 jijini Moscow na kuhudhuriwa na Mabalozi wa nchi mbali mbali wanaowakilisha nchi zao nchini Urusi hususan wa nchi za Afrika na Sub-Sahara, viongozi wa Serikali ya Urusi, Viongozi na wafanyakazi wa Mashirika mbali mbali ya Urusi yanayojishughulisha na mambo ya Utalii na usafirishaji na wananchi mbali mbali. Vile vile Mashirika ya usafiri ya nje kama Ethiopian Airlines n.k

  • Mhe. Balozi Mumwi akiwa na Mabalozi wa nchi za Afrika kwenye kukata keki katika hafla hiyo, kuonesha ishara ya Ushirikiano na Upendo katika Mambo mbali mbali ya Kimaendeleo na Kijamii
  • Mhe. Balozi Mumwi akiongea jambo na Mhe. Nomasonto Maria Sibanda - Thusi, Balozi wa Afrika Kusini katika Shirikisho la Urusi katika hafla hiyo
  • Mhe. Balozi Mumwi akitoa Cheti (Certificate of Appreciation) kwa Prof. Nelly Gromova, Mwenyekiti wa Chama cha Kiswahili Moscow (CHAKIMO) kwa jitihada kubwa anazochukuwa katika kukuza lugha ya kiswahili hapa Moscow
  • Mhe. Balozi Mumwi akitoa cheti (certificate of Appreciation) kwa mwakilishi wa Kampuni ya "Masai Shuka" kwa kuitangaza vyema Tanzania kupitia sanaa na Utamaduni
  • Waheshimiwa Mabalozi na wageni waalikwa wengine wakiangalia bidhaa mbali mbali za asili kama Masai Shuka na nyenginezo
  • Waheshimiwa Mabalozi na waalikwa mbali mbali wakifurahia kunywa kahawa ya Tanzania katika maonesho ya Bidhaa za Tanzania yaliyofanyika siku hiyo
  • Pichani ni wanafunzi wanaosoma Kiswahili kutoka Chama cha Kiswahili Moscow (CHAKIMO) wakionesha Umahiri wao wa kuongea lugha ya Kiswahili ikiwemo kusoma mashairi ya kumsifu Shaaban Robert
  • Jinsi Meza zenye bidhaa mbali mbali za Tanzania zilivyopendeza siku hiyo katika maonesho ya Utalii, Bidhaa za asili, sanaa na Utamaduni wa Tanzania
  • Mhe. Balozi Maj. Gen. (Mst.) Simon M. Mumwi akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Wafanyakazi wa Ubalozi pamoja na wanafunzi wanaosoma katika Shirikisho la Urusi waliohudhuria katika hafla hiyo
  • Mhe. Balozi Mumwi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi pamoja na wageni waalikwa katika hafla hiyo