Ubalozi wa Tanzania kwa Kushirikiana na Kampuni ya "Coral Travel" uliandaa hafla ya uzinduzi wa Safari za "Coral Travel" nchini Tanzania tarehe 21 Februari 2019. Kufuatia uzinduzi huo Kampuni ya "Coral Travel" ambayo inajihusisha na usafirishaji wa Watalii  kwenda nchi za kiafrika sasa itaanza safari za kupeleka watalii Tanzania hususan sehemu ya Ukanda wa Kaskazini (Nothern Circuit) na Zanzibar. Meneja wa Kampuni hiyo Bi. Ilya Derin alisema Program hiyo inatarajiwa kuanza kabla ya mwezi Juni 2019